Jumatatu 6 Oktoba 2025 - 15:40
Maandamano ya Kimataifa yaongezeka kwa Kasi kwa ajili ya Kuiunga Mkono Ghaza na Kulaani Utekaji wa Flotilla ya S‌umūd‌

Hawza/ Baada ya utawala wa Kizayuni kuiteka meli iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ghaza, kwa jina la Flotilla ya S‌umūd‌, watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wameandamana katika nchi nyingi wakitaka vichukuliwe vikwazo vikali na madhubuti zaidi dhidi ya Israel.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, katika mabara yote duniani, wafuasi wa Palestina walimiminika mitaani kulaani kitendo hiki cha jinai kilichofanywa na Israel dhidi ya ubinadamu. Israel, ambayo ni mhalifu, kwa kuzingira meli 41 na takriban watu 400, imezuia kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa watu wanyonge wa Ghaza.

Huko Barcelona, takribani watu 15,000 waliandamana wakioza sauti zao kwa kauli mbiu isemayo: “Watu wa Gaza, ninyi hampo peke yenu.” Ada Colau, aliyekuwa Meya wa zamani wa Barcelona, alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakielekea Ghaza ndani ya meli za misaada na alitekwa na utawala katili wa Kizayuni. Yeye pamoja na wanaharakati wengine wa haki za binadamu — wakiwemo wajukuu wa Nelson Mandela waliokuwa ndani ya meli — walikamatwa na kufukuzwa na Israel.

Aidha, idadi kubwa ya waandamanaji walikusanyika mbele ya Bunge la Ireland katika mji wa Dublin kuonesha hasira zao dhidi ya hatua ya Israel kuzuia kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu Ghaza — eneo linalojulikana kwa historia ya mapambano ya Wairishi dhidi ya ukoloni wa Uingereza.

Bi Miriam McNally, ambaye binti yake alikuwa ndani ya moja ya meli hizo, katika mkutano huu alisema katika mahojiano: “Ni kweli nina wasiwasi kwa ajili ya binti yangu, lakini kwa kweli najivunia yeye sana.”

Paris pia ilishuhudia maandamano ya maelfu ya watu, na takribani waandamanaji 100 walikamatwa na polisi wa Marseille.

Huko Italia, ambapo watu walikuwa wakitaka kufungwa kwa bandari, maandamano mengi ya kupinga hatua ya Israel yalifanyika. Mji wa Rome peke yake ulijionea maandamano ya watu 10,000.

Chanzo: Al Jazeera

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha